USIKU WA KIFO (04)

Jina.......Usiku Wa Kifo
Mtunzi....Dully Official Tz
WhatsApp....0752748344
Mkasa wa kutisha...

Sehemu ya 04

ILIPOISHIA..

"Tony nishike mkono...!!
       Niliongea huku nikikimbia kwa tabu sana maana nilikuwa tayari nimeanza kuchoka basi Tony alipunguza kasi ya kukimbia na kunisubiri lakini kitendo cha kumfikia Tony nilipigwa na mkuki wa mgongo ambao ulinipa maumivu makali sana na kuanguka chini......ENDELEA

Nguvu ziliniisha hapo hapo, sikuweza kuinuka tena kukimbia niliregea mwili na kupoteza fahamu lakini nilikuja kuzinduka baadae sana nlijikuta kwenye jumba moja kubwa lililochakaa nimelala na mgongoni nikiwa nimefungwa bandage.

Haraka niliinuka na kuangaza huku na kule lakini nikiwa kwenye maswali mengi nilimuona Tony akiingia huku ameshika bega lake ambalo lilikuwa na jareha kubwa sana.

"oh! Mungu mkubwa hatimae umeamka Raiyan vipi unaendeleaje na hali?"
      Tony aliniuliza lakini sikumjibu nilibaki na maswali je alimisaidiaje kwenye tukio lile inamaana amepambana na yule mtu wa ajabu au vipi?.

Sikupata jibu kwa wakati huo niliinuka na kumfuata Tony huku nikimuuliza juu ya wenzetu ambao walikimbia kwa njia yao.

"Hata mimi sifahamu nimetoka kuwatafuta ila sijawaona lakini naimani watakuwa salama"
     Tony alinijibu huku akikaa chini na mimi nilipozungusha macho pande zote za jengo hilo nilipata kutambua kwamba ile ilikuwa hospital ya zamani.

"Ok ni jambo la kumuonga mungu wawe salama na sisi inabidi tukae chini tuangalie tutajikombiaje la aivyo tutaishia humu humu"

Nilisogea kando ya Tony na kuketi, nilitoa kitambaa changu mfukoni na kumfunga kwenye jeraha lake ambalo lilionesha amejeruhiwa kwa kitu chanye ncha kali.
       Tulikaa hapo tukipiga story lakini story ziliponoga nilianza kuhisi njaa na tumbo langu lilianza kuunguruma.

"Pole sana najua una njaa kwahiyo nakuomba unifuate kuna sehemu nimeona mti wa matunda naimani tukipata matunda njaa itapungua hebu nifuate"

Niliinuka na kutoka nnje kumfuata Tony lakini muda wote nilikuwa na hofu sana maana kwa tukio lililotokea masaa machache nyuma lilizidi kunitia woga.
     Safari yetu ilikomea kwenye mti mkubwa wa maembe hapo tulisimama na kuutazama kwa sekunde kadhaa kisha Tony alipanda na kuangusha maembe machache ambayo tungeyatumia kula na siku hiyo ikapita salama.

Baada ya kupata matunda tulirudi kwenye ile hospital lakini kabla hatujaingia ndani tuliona kichwa cha Michael kikiwa mrangoni.

"Mungu wangu..!!"
      Woga ulinipanda na kuanza kurudi nyuma lakini Tony alinishika mkono na kunisogeza karibu yake.

"Hawa watu sijui majini tayari wamejua tulipo kwahiyo sehemu hii sio salama tutafute sehemu nyingine ya kupumzika kwa muda tule na baada ya hapo tuwatafute wenzetu tuondoke"

Wazo la Tony sikulipinga tulitoka pale na kuzidi kusonga mbele kuangalia uwezekano wa kupata sehemu ya kupumzika kwa muda, tule matunda yetu na safari ya kutafuta wenzetu ianze.

                             ********

Safari yetu tulifika kwenye pango moja na kusimama hapo, tulilitazama kwa muda lile pango kisha Tony aliniomba tuingie ili kupata kupumzika hapo.

"Tony unasema nini wewe yaani tuingie humu alafu kulivyo kunatisha mh hapana mimi siingii kama itawezekana tutafute sehemu nyingine lakini sio humu"

"Acha nikwambie Raiyan humu ni salama kabisa kama hutaki mimi nitatangulia wewe kaa hapo likitokea la kukutokea mimi sihusiki"
       Maneno ya Tony yalinitisha sana nilitazama nyuma na kujikuta nikiogopa hapo sikuwa na pingamizi nilimfuata Tony na wote tuliingia humo.

Pango lile kwa muonekano wa nnje lilikuwa dogo sana lakini kwa ndani lilikuwa na uwazi mkubwa basi tuliketi kwenye mawe makubwa yaliyokuwa mule story zilianza huku tukila maembe bila maji wala kito chochote cha kushushia.

"Hivi Raiyani wewe kwa mtazamo wako unaona tutatoka humu maana mimi nimekata tamaa kabisa ya kutoka na kuishi"

"Usiseme hivyo alafu tambu wewe mtoto wa kiume kwahiyo kama umekata tamaa mapema je mimi itakuwaje wakati wewe ndiyo unatakiwa uwe mfano kwangu kuhakikisha una....."
      Kabla sijamaliza kuongea tulisikia vishindo nnje na dakika za kuhesabu waliingia watu mule mule tulipokuwa sisi na muda huo Tony alikuwa amezima tochi kwahiyo kiza cha mule hatukuweza kuwaona wala wao hawakutuona.

Watu wale walionekana walikuwa wakikimbizwa maana walihema kama wana riadha ambao walikuwa wakingombania medali ya dunia.

"Jamani sijui Raiyan na Tony watakuwa wapi na hatuelewi kama ni wazima au wamekufa"
      Sauti hiyo ilikuwa ya Sara na baada ya sisi kusikia hivyo Tony aliwasha tochi na kuwafanya wakina Sara washtuke.

"Msishtuke ni sisi"
     Niliongea kuwatoa hofu lakini nilipomtazama betina mguuni alikuwa akivuja damu nyingi na mguu wake mmoja ulikuwa umekatika.

"Munguuuu...!! Betina ndiyo umekuwa hivi?"

"We acha tu hapa nina maumivu makali ila najikaza tu"
       Betina aliongea bila wasi ila mimi nilimuonea huruma niliinuka ili kuondoka lakini Tony alinishika mkono.

"Unataka kwenda wapi wakati huko nnje ni hatari sana"

"Naenda kuchukua dawa kwenye lile jengo la hospital wewe huoni kama Betina anapoteza damu nyingi"

"Basi twende wote"
       Tony alitaka kuinuka lakini nilimzuia nilichukua tochi aliyokuwa ameshika na kutoka nnje kwa tahadhari kwenda kuchukua dawa kwenye ile hospital ambayo tuliona kichwa cha Michael.

                           ********

Safari yangu ilijaa umakini mkubwa sana nilitembea kama askari wa vita mwisho nilifika kenye ile hospital lakini kichwa cha Michael sikukiona tena.

"Mungu nisaidie nitoke salama nakutegenea wewe tu"
     Hofu yangu na wasi wasi wote niliukabidhi kwa Mungu nilijikaza na kuingia ndani.

Nilipita kila chumba na kufungua makabati lakini sikuona kitu ila wakati nataka kutoka niliona chumba kimoja ambacho hicho sikuingia kabla, nilikisogelea na kufungua.

Chumba hicho kilikuwa kikubwa sana kilikuwa na madawa mengi pia kilikuwa na mifupa mingi ya binaadamu nilisita kidogo lakini roho ya ujasiri iliponiingia nilipiga hatua kuingia ndani zaidi.

Kila dawa ambayo niliihitaji niliikuta mule basi nilichukua dawa nilizohitaji na kutoka nnje ila wakati nataka kufunga mrango nilisikia nikiitwa kwa jina langu na aliekuwa akiniita sikumuona.

"Nani tena ananiletea mauzauza mbona anataka kuniua kwa presha majani"
       Sikutaka tena kuufunga ule mrango niligeuka na kutoka eneo hilo lakini nikiwa kwenye korido ya kutoka nnje nilikutana uso kwa uso na mtu wa ajabu.

Mtu yule hakuwa na tofauti na watu wale waliotukimbiza mwanzo ila huyu alikuwa mrefu tu na alionekana kuwa mwenye nguvu sana.
      Yule mtu aliponiona alicheke sana hapo nikajikuta nikitetemeka na kuangusha dawa chini.

"Na..na..naomba niende mimi sikuja kwa ubaya naomba niende tafadhali"
      Nilianza kutetemeka huku nikiomba kuachwa lakini yule mtu hakujali alichomoa kisu chake kilichokuwa kiunoni na kuanza kunisugelea huku nikirudi nyuma kwa hofu.

"Raiyani pambana kama mwanamke ukilegea tu umekufa huyo mtu hayupo kimasihara kabisa"
      Nilijiwazia na kutazama pembani niliona mkasi haraka niliuokota na kuushika kwa mikono miwili.

"Naomba usisogee kama utasogea nakuuwa najua unapenda maisha yako sasa ili nisikuue nipishe nipite"

Niliongea kwa ujasiri uliojaa woga lakini lile jitu halikutaka kunisikiliza lilinisogelea na kunikaba shingoni, nilipojaribu kufurukuta nilichomwa kisu cha tumbo na kupelekea damu nyingi zianze kunitoka....ITAENDELEA...

Mh....!!? Mambo ni magumu kwa Raiyan jamani sasa hata sielewi nini kitafuta mh.!! hebu tusubiri sehemu ya 5 tupate majibu..

COMMENT, SHARE NILETE MIENDELEZO


 

Comments

Popular posts from this blog

JERAHA LA MOYO (02)

JERAHA LA MOYO (1)

USIKU WA KIFO (03)