JERAHA LA MOYO (1)

  

Sehemu Ya 01

Mtunzi : Dully Tz

WhatsApp :0752747344

Ilikuwa asubuhi na mapema siku ambayo Nelson alikuwa na furaha sana siku hiyo ilikuwa ni siku ambayo alikuwa akienda kuanza kidato cha kwanza baada ya kuhitimi elimu ya msingi na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya secomdary hivyo kwa siku hiyo alikuwa na furaha isiyo kifani.

Aliamka majira ya saa kumi na moja subuhi na kujiandaa kisha alienda chumba cha mama yake na kusimama nnje ambapo alianza kubisha mrango.

"Hodiii mama..!!?"

Nelson aliita huku akiwa na shakuku kibao na kweli mama yake alifungua mrango na kumkuta tayari amejiandaa kama mwanafunzi.

"Heeee jamani asubuhi yote hii hata shule wanafunzi hawajaanza kwenda wengine wanavuta mashuka wewe tayari umeshavaa na safari juu ya kutaka tuondoke"

"Ndiyo mama sitaki kuchelewa mimi nikakosa dawati la kukalia"

"Hahaha amna kwanza kule hakuna madawati kama shule ya msingi yaani kule unapewa kiti kila mmoja na chake'

"Mh mama ila nataka kuwahi na namba pia nisije kuchapwa"

"Ah akuchape nani wewe kalale ikifika saa moja kamili nakuja kukuansha tuondoke"

Kweli Nelson alirudi kitandani na kwakua alikuwa na usingizi alioukatisha basi usingizi ulimchukia mpaka alipokuja kuamshwa na mama yake mida ya saa mbili kamili.

"Haya Neli muda ndiyo huu nawa uso tuomdoke niwahi kurudi niende kazini"

Nelson aliamka haraka na kufanya kama alivyoelekezwa hapo safari ilianz kujipakia kwenye gari lao na kuodoka.

"Hivi mama Secondary tunachapwa kama shule ya msingi"

Nelson akiwa kwenye gari alimtupia mamayake swali ambalo lilimfanya atabasamu.

"Kule unachapwa kama kawaida tena ukileta ujinga na ukorofi utachapwa kila siku ila muhimu nataka uwe na adamu kwa wenzako pia nataka usome sana sawa"

"Sawa mama"

Basi safari iliendelea na kwakua hakukuwa na umbali sana walifika shuleni pale majira ya saa mbili na robo kisha kufanya utaratibu wa kushuka ili kwenda kuripoti kwa mwalimu mkuu.

Harakati zote zilifanyika Nelson kwakua alikuwa amechelewa kidogo alikuta darasa A limejaa hivyo aliamuriwa aingie darasa B na kujumuika na wenzake ambao aliwakuta mule.

Nelson alikuwa ni kijana wa miaka 17 pia kijana Nelson alilelewa na mama pekee baada ya baba kuachana na mama yake kisha kuoa mke mwengine.

     Mama Nelson alibarikiwa watoto wawili mmoj wa kike ndiye wa kwanza aliekuwa chuo anafata Nelson ambae yeye yupo form one.

Basi alifika darasanu na kwakua hakukuwa na watu wengi maana wengie walichelewa kuripoti basi alipata kiti sehemu ya pekeyake na kuketi huku akiwa hana habari na mtu yeyote.

       Hakutaka kukaa hivi hivi alitoa kitabu chake kidogo cha katuni na kuanza kukisoma huku skisubiri masomo yaanze.

                           **********

Inatimia saa tatu kamili wanafunzi wote walimalizika kusajiliwa hivyo mwalimu aliingia darasani na kuanza kuwauliza maswali kabla ya yote.

"Marahaba wanafunzi mimi naitwa madam hawa ni mwalimu wa kiswahili hivyo kabla sijaanza kuwafunsha nilikuwa naomba mjitambulishe mmoja baada ya mwingine"

Kweli wanafunzi walianza kujitambulisha na kufanya kila mmoja amjue mwenzake kwa jina.

Zamu ya Nelson ilifika alijitambulisha lakini katika sehemu aliyokaa alikuwa pekeyake hivyo mwalimu hawa alimuamisha na kumuwela dawati la mbele yale ambapo kulikiwa na mwanafunzi mmoja tu.

"Daaah siamini nimekaa na wakishua"

Nelson alipokaa pale alipoambiwa alipokelewa na maneno ya mwanafunzi yule alieambiwa akae nae hivyo alijikuta akichukia sana lakini hakuwa na jinsi.

"Ila jina hilo silitaki ukitaka nikuharibu endelea na upuuzi huo"

Nelson hakuwa mpole kiivyo alimchimbia mkwara mzito yule mwanafunzi mpaka mwalimu hawa aliwaona.

"Hey Nelsona na Frank kuna nini hapo"

Nwalimu hawa aliuliza huku akiwa amekamata kiboko na kuwasogelea.

"Mwalimu mimi naona nirudi sehemu yangu maana siwezi kukaa na mtu kama huyu"

Kweli Nelison alibeba begi lake na kurudi alipokaa mwanzo huku akiwa na hasira.

                           **********

Week mbili zilikatika masomo yaliendelea kama kawaida huku Nelson akipata rafiki alieshibana nae sana alieitwa Yassin kiufupi yeye na rafiki yake walipendana sana pia hata kutembea walikuwa wakitembea pamoja lakini walikuja kuachana kwenye kitio cha gari ambapo kila mmoja alikuwa akipanda gari la kuelekea kwao.

"Hivi Nelson unajua mimi yule Farank ananiboa sana"

"Sio wewe tu hata mimi sijui kwa nini kama jana naingia darasani nakuta kachukua begi langu na kurushiana na yule demu sijui Neyla sasa ipo siku nitamzingua"

"Ah achana nae unajua ukipigana unaweza kusimamishwa shule"

"Ni sawa ila kazidi sana mpaka ananikera yaani au kwasababu anamiguu ile mirefu iliyoenda hewani anajua nitamuogopa mimi namzingua"

"Ah acha nae dawa yake inachemka"

Basi marafiki hao waliendelea kupiga story huku wakipata chakula maana muda huo ulikuwa muda wa break hivyo wanafunzi wote walikusanyika migahawani.

Wakiwa pale wakijadili alikuja mdada mmoja aliefahamika kama  hadija na kusimama mbele yao.

"Nyie kaeni tu kule kwenye kiti cha Nelson kuna mtu kakaa tena anaonekana mgeni sijui kaja leo"

Nelson aliposikia hivyo aliokota bagi lake na kukimbilia darasani ili kujua nani amekaa sehemu yake hata ikiwezekana amtoe ila alipofika mule alijikuta akiishiwa pozi baada ya kukuta mgeni mwenyewe wa kike tena alikuwa ametulia hata wasi hana.

"Hivi huyu cheupe kwani hajaona sehemu za kukaa mpaka akae kwangu sasa muache namtoa hata simuogopi"

Nalson alijikaza kisabuni japo alikuwa na aibu lakini alivumilia na kumsogelea yule mwanafunzi mgeni........!! ITAENDELEA

simulizi mpya naombeni support zenu kukamilisha simulizi hii..

Usisahau kulike page yangu facebook (Simulizi Za Dully)


Comments

Popular posts from this blog

JERAHA LA MOYO (02)

USIKU WA KIFO (03)