USIKU WA KIFO (03)
Jina.......Usiku Wa Kifo
Mtunzi....Dully Official Tz
WhatsApp....0752748344
Mkasa wa kutisha...
Sehemu ya 03
ILIPOISHIA..
Mpenzi msomaji yaani asikwambie mtu usingizi wa hapo ulikuwa mtamu sana lakini nikiwa kwenye usingizi nilishtuka baada ya kuitwa kwa jina langu na nilipoamka sikuwaona wenzangu wote walikuwa wametoka nnje na vilio ndivyo vilikuwa vikisikika upande wa nnje....ENDELEA...
Niliinuka haraka na kutoka nnje lakini sikuamini kuona damu zimetapakaa chini tena zilikuwa kwa mtindo wa kuburuzika kuashiria aliekufa alikuwa akiburuzwa kupelekwa sehemu nyingine.
"Jamani kwani kuna nini na hizi damu ni zanani"
Niliuliza kwa hofu lakini sikujibiwa ila nilioneshwa ishara kwa kidole nitazame mbele na nilipotazama niliona nguo za dereva wetu zikiwa juu ya mti.
"Mungu wangu ni nini tena hiki..!!?"
Hofu niliyokuwa nayo nilihisi kizungu zungu lakini tukiwa kwenye majonzi Tony alitushauri kitu.
"Jamani mimi siamini kama kweli dereva wetu amekufa sasa ili kupata ushahidi naombeni tuifuae hii damu tuone imeishia wapi"
Tony aliongoza njia akifuatiwa na wenzangu lakini mimi nilisita na kukataa kwenda kabisa.
"Sasa unakataa kwenda kwanini je hata tukisema tuondoke unaweza kuendesha gari wewe ok kaa hapo hapo likikukuta la kukukuta sisi hatuhusiki"
Aron baada ya kusema hayo nilijikuta nikiingiwa na hofu sana niliwasha tochi yangu na kuwafuata lakini muda wote bado nafsi yangu ilisita kabisa.
Safari yetu kuifuatisha ile michirizi ya damu ilikuwa defu sana, tulitembea takribani dakika 10 na mwisho tulifika kwenye mti mmoja hapo tuliona damu nyingi sana na ule mburuzo ulikuwa umeishia hapo.
Tuliangaza huku na kule lakini hatukuona kitu mwisho tulikata shauri na kugeuka ili kurudi tulipotoka tukaangalie taratibu nyingine za kuondoka kwenye mji huo.
"Jamani hebu tazameni kule juu"
Michael yeye ndiye aliekuwa wa mwisho na alipotuambia hivyo tuligeuka na kumuona akimulika tochi yake juu ya mti ilibidi wote tuinue vichwa vyetu kuangalia ni nini ambacho alikiona Michael.
"Mamaaaaaa...!!?"
Mabinti wote tuliokuwa pale tulijikuta tukipiga kelelel na kukimbia hovyo lakini Tony na wenzake hawakutaka kutetereka walibaki kutazama juu ambapo kulikuwa na maiti ya dereva wetu ikiwa imefungwa juu na tumbo lake likiwa limechanwa huku utumbo ukining'inia kama nyana iliyokuwa buchani.
Kiukweli tukio lile lilikuwa geni kwangu nilikuwa nikiona kwenye runinga tu ila leo baada ya kushuhudia live nilijikuta nikitapika na kuishiwa nguvu.
"Jamani sasa kukimbia na kulia sio suluhisho ila tunachotakiwa kufanya hapa ni kitu kimoja tuishusheni hii maiti tuizike alafu tuangalie utaratibu wa kurudi chuo maana sio salama tena huku"
Tony maneno yake yalikuwa ya muhimu sana na wao kama wanaume walishirikiana kuishusha ile maiti na baada ya mumaliza tulichimba shimo dogo kwa kutumia miti kisha kumfukia na kumpa heshima ya mwisho.
"Sasa jamani tumemaliza maziko hapa tuangalieni utaratibu wa kurudi tu hata kama hakuna anaeweza kuendesha gari mimi nitajitahidi ili tu kutoka humu"
Aron alianza kuongoza njia kurudi tulipotoka lakini njia nzima tulikuwa kimya maana kiza kilikuwa kinene pia licha ya kuwasha tochi zetu lakini bado kulikuwa kunatisha.
********
Mungu alijaalia tulirudi salama sehemu ambapo tuliweka kambi lakini tulipoingia hatukuona mabegi wala kitu chochote ambacho kilituhusu na kilichotufanya tushangae zaidi ni baada ya kuona maiti ya dereva wetu ikiwa pale.
Mpenzi msomaji wa mkasa huu yaani hakuna siku niliyochanganyikiwa kama siku hiyo yaani nilihisi kupandwa na kichaa ambacho sikuelewa kilikuwa kikitoke wapi.
"Jamani hapa sio salama tena inabidi tuondokeni haraka la sivyo kitakachotukuta ni kikubwa sana"
Tony akituambia na kuanza kuondoka lakini wakati tunatoka kwenye mjengo huo Michael alikuwa wa mwisho kutoka na mrango wa jengo hilo ukijifunga akiwa ndani.
"Jamani nisaidieniiiiii...!!!"
Sauti ya Michael ilisikika kutokea mule ndani ilibidi wote tugeuke na kurudi ili kwenda kutoa msaada lakini kitendo cha kuufikia mrango ukimya ulitawala na damu ndiyo zilikuwa zikitiririka chini ya mrango kutokea ndani.
Hakuna alieamini kila mmoja alikimbia kunusuru maisha yake lakini mimi sikuweza kukimbia tena nilikaa chini na kuanza kulia maana hata nguvu ya kukimbia sikuwa nayo tena.
"Raiyan hebu tuondoke utakuja kufa sio salama tena hapa"
Tony alikuwa tayari amekimbia lakini alipogeuka na kuniona bado nimekaa chini alinifuata na kuniinua tutoke maeneo hayo.
Mbio zetu zilikuwa za muda mrefu sana tulitumia kama masaa matatu kufika kwenye gari letu lakini tulipofika hatukuamini kukuta maiti ya Michael ikiwa nje ya gari na gari pia lilikuwa limetobolewa matairi kuashiria hakuna mtu kuondoka.
"Mungu wangu Michael"
Betina alikuwa akimpenda sana Michael na kilichomfanya ampende zaidi ni upole wake kiufupi Michael alikuwa mpole sana na mwenye roho nzuri ila kwa kifo alichokufa hapo kilikuwa ni kibaya sana.
Maiti ya Michael haikuwa na kichwa aliuwana na kutolewa kichwa chake au naweza kusema alichinjwa kama kuku na mpaka muda huo hatukujua nani anafanya tukio na chanzo ni nini mpaka tuandamwe kiasi hicho.
"Jamani hapa tunatakiwa tuwe majasiri tuzikeni hii maiti na kuangalia utatatibu wa kuondoka"
"Tony sasa tutaondokaje wakati matairi ya gari yote yametobolewa hakuna cha kufanya tusubiri kufa tu"
Maneno yangu yaliwafanya wote waanglie matairi ya gari na baada ya kuhakikisha kile nichosema walijikuta wakiishiwa nguvu na kukaa chini kabisa.
Tulikaa kama dakika kadhaa kisha tulisimama na kuchukua maiti ya Michael ambayo tulikwenda kuitupa kweny mto wa ahadi na baada ya kukamilisha yote tulichukua vichache vilivyosalia kwenye gari na kuondoka zetu mbele kwa mbele.
*********
Safari isiyo na matumaini ilianza hapo tulikuwa tukitembea bila kufahamu tunaenda wapi lakini tukiwa kwenye pita pita zetu tulisikia sauti ya kengele iliyotufanya tusimame.
"Jamani hiyo si kengele ya kanisa hebu tufuateni sauti huenda tukapata msaada huku"
Niliongoza njia kuelekea mahali iliposikika kengele lakini Aron alinishika mkono na kunirudisha.
"Huko ni kujitakia kufa kwa lazima Raiyan tambua mpaka sasa tumepoteza watu wawili na waliowaua hawafahamiki sasa unataka kwenda huko unawaamini vipi?"
Maneno ya Aron yaliniingia akilini nilijikuta nikiwa mpole na kuongoza safari kuifuata barabara ya gari lakini tukiwa kwenye safari yetu ghafla tulisikia mchakacho nyuma yetu na tulipogeuka hatukuamini kuona watu wa jabu sana.
Watu hao walikuwa wawili na sijui niwaelezee vipi, walikuwa kama mashetani wenye sura mbaya huku mikononi walikuwa wameshika mapanga na mikuki hii ilitufanya kila mmoja kukimbia njia yake ili kujinusuru.
Bahati nzuri nilikimbia njia moja na Tony ila Aron, Betina, Sara na Salome alikimbia njia moja na sikufahamu walikuwa wamepitia wapi maana kila mmoja alikuwa na hofu ambayo hakutaka kumfutilia mwenzake.
"Tony nishike mkono...!!
Niliongea huku nikikimbia kwa tabu sana maana nilikuwa tayari nimeanza kuchoka basi Tony alipunguza kasi ya kukimbia na kunisubiri lakini kitendo cha kumfikia Tony nilipigwa na mkuki wa mgongo ambao ulinipa maumivu makali sana na kuanguka chini......ITAENDELEA
Unafikiri nini kitafuta hapo kwa Raiyna na Tony..!!? mimi sina majibu ila majibu itapayata sehemu ya 4
LIKE, SHARE KWA WINGI NILETE SEHEMU YA 4

Comments
Post a Comment