JERAHA LA MOYO (02)

JERAHA LA MOYO
Sehemu Ya 02
Mtunzi : Dully Tz
WhatsApp : 0752747344

ILIPOISHIA.....

"Hivi huyu cheupe kwani hajaona sehemu za kukaa mpaka akae kwangu sasa muache namtoa hata simuogopi"

Nalson alijikaza kisabuni japo alikuwa na aibu lakini alivumilia na kumsogelea yule mwanafunzi mgeni........!!ENDELEA....

Nelson mbwembwe zote alizokuwa nazo lakini alifika pale na kujikuta amepowa ghafla baada ya macho yake kugongana na yule binti mweupe.

"Am ah ila samahani kama nitakuwa nakusumbua hivi wewe ni mwanafunzi mpya kwenye darasa hili sio"

Nelson aliamua tu kupotezea na kuanza kuongea mambo tofauti na aliyopanga mwanzo.

"Ndiyo mimi mgeni nimekuja leo"

"Ahaaa sawa ila ulifaulu hapa hapa au umeamishiwa"

"Hapana nimetoka tanga nimeamishiwa hapa ila nilitakiwa niripoti jana lakini kuna dharura ilitokea sasa nimeletwa leo'

"Ahaaa ok karibu mimi naitwa Nelson sijui wewe"

Nelson aliongea huku akimpa mkono yule binti lakini hakutaka kupokea alibaki kimya tu akimtazama mpaka pale Nelson alipoona aibu na kushusha mkono wake.

"Ok samahani kwa kukusumbua kwaheri"

Nelson alitoka nnje huki akiwa na aibu kibao kwanza alikataliwa kupewa mkono pia hakutajiwa jina yaani kiufupi kwake aliona kama dharau na fedheha.

"Oya vipi mbona umerudi mnyonge sana umezinguliwa na Frank nini?"

Yassin alimtupia swali Nelson baada ya kumuona amerudi akiwa mnyonge tofauti na alivyokwenda.

"Ah amna nipo kawaida ila kuna demu mgeni ameingia class sasa ndiyo amekaa sehemu yangu"

"Kwahiyo sasa inakuaje au kama vipi kamwambie teacher hawa akupeleke darasa "E"

"Ah wewe mwehu kweli yaani nikasome E ah bora nikae chini kuliko kwenda E lakini ndiyo hivyo huyo demu kwanza ana zarau kinoma tofauti na muonekano wake"

"Kivip mbona bado sijakuelewa"

"Ah eti nafika pale nampa mkono na kumuuliza jina ananikata jicho kama kinyesi yaani"

"Ah achana nae ila niachie mimi nikiingia namtoa atakaa chini kwani shule ya babake hii"

Basi wakati wanaendelea kumjadili huyo mwanamke mgeni kengele ya kurudi madarasani ilisikika hivyo kila mmoja hakuwa na budi kuacha alichokuwa akikifanya na kurudi class.

Yassin na Nelson walifika mpaka mrangoni na kusimama nnje ya darasa lao wakijadili jambo.

"Sasa mwanangu tukiingia tutamtoaje maana namuonea huruma ujue alafu mgeni"

"Wewe niachie mimi nitamtoa tu"

Kweli waliingia kwa lengo hilo lakini walipofika mule walishangaa kutomuona yule mwanafunzi mgeni.

"Mh mbona hayupo au atakuwa umeniongopea"

"Amna alikuwa humu humu labda ametoka nnje au kahamishwa darasa"

Kweli yule mwanafunzi hawakumuona tena mpaka anaingia mwalimu wa mathematics (hisabati) na kutaka kufundisha.

"Jamani mbona ubao hamjafuta mpka sasa hebu Nelson inuka kachukue kifutio darada C uje ufute na kuanzia leo wewe utakuwa monitor wa darasa"

Nelson alistaajabu kuanbiwa hivyo ila hakuwa na jinsi alitoka mpaka darasa C kwenda kuchukua kifutio lakini alipotupa macho kwa wanafunzi alishangaa kumuona yule mwanafunzi mgeni akiwa darasa lile.

Hakutaka kumshangaa sana alichukua kifutio na kurudi darasani kuendelea na masomo kama kawida.

"Oya Yassin kumbe yule demu yupo darasa C"

"Kweli au"

"Kweli wewe ukitoka twende ukamuone"

"Ok basi powa aina noma"

                          **********

Muda ulisogea majira ya saa nane baada ya kengele kugongwa wanafunzi walikusanyika mstarini na hiyo iliashiria kulikuwa na matangazo yanatakiwa kuwafikia wanafunzi.

"Habarizenu watoto"

Mwalimu mkuu alianza kwa salamu baada ya wanafunzi kuitika na kumsalimia alikohoa kidogo na kuendelea.

"Sasa leo nilikuwa nina maongezi na nyie machache maana muda auruhusu na jua kama mnavyoona linawachoma sasa nitawaambia machache kesho walimu wenu watawatangazia madarasani"

Wanafunzi bado waliendelea kuwa kimya ila muda huo wote yule binti mgeni macho yote yalikuwa juu ya Nelson na alionekana mwenye sura ya huzuni pia alikuwa kama na shauku ya kutaka kumwambia kitu Nelson ila alijizuia.

"Basi leo tunafungua mashindano rasmi pia shuleni kwetu haturuhusu mchezo wa mpira wa miguu sasa kesho tutakuwa tunasajili wanafunzi wanaotaka kushiriki riadha hivyo kama utahitaji walimu watapita madarasani na kuanza kuwasajili kwahiyo ijumaa mashindao rasmi yataamza"

Basi wanafunzi siku hiyo walijawa na furaha hasa kwa form one maana wao ndiyo walikuwa mwaka wao wa kwanza pia ratiba ile ilikuwa ngeni kwao hivyo waljikuta na furaha sana mpaka walipokuwa wakirudi makwao njiani waliongelea jambo hilo.

Yassin na Nelson waliongozana kama marafiki na kama kawaida yao huku wakipiga story kuelekea kituoni kupanda gari.

"Nelsoooon...!!?"

Nelson akiwa njiani na Yassin sauti ya kike kutokea nyuma ilisikika na kufanya wote wageuke kutazama alikuwa ani nani.....!!?ITAENDELEA...

Hakikisha una comment ili kupata miendelezo (3)


 

Comments

Popular posts from this blog

JERAHA LA MOYO (1)

USIKU WA KIFO (03)