Posts

JERAHA LA MOYO (02)

Image
JERAHA LA MOYO Sehemu Ya 02 Mtunzi : Dully Tz WhatsApp : 0752747344 ILIPOISHIA..... "Hivi huyu cheupe kwani hajaona sehemu za kukaa mpaka akae kwangu sasa muache namtoa hata simuogopi" Nalson alijikaza kisabuni japo alikuwa na aibu lakini alivumilia na kumsogelea yule mwanafunzi mgeni........!!ENDELEA.... Nelson mbwembwe zote alizokuwa nazo lakini alifika pale na kujikuta amepowa ghafla baada ya macho yake kugongana na yule binti mweupe. "Am ah ila samahani kama nitakuwa nakusumbua hivi wewe ni mwanafunzi mpya kwenye darasa hili sio" Nelson aliamua tu kupotezea na kuanza kuongea mambo tofauti na aliyopanga mwanzo. "Ndiyo mimi mgeni nimekuja leo" "Ahaaa sawa ila ulifaulu hapa hapa au umeamishiwa" "Hapana nimetoka tanga nimeamishiwa hapa ila nilitakiwa niripoti jana lakini kuna dharura ilitokea sasa nimeletwa leo' "Ahaaa ok karibu mimi naitwa Nelson sijui wewe" Nelson aliongea huku akimpa mkono yule binti lakini hakutaka kupokea ...

USIKU WA KIFO (04)

Image
Image
Jina....NYUMBA YA MAJINI Mtunzi....Dully Official Tz WhatsApp....0752747344        Sehemu....01         Katika maisha tunayoishi tunaishi na viumbe vingi sana ukiachana na viumbe vya kuonekana pia tunaishi na viumbe ambavyo havionekani kama majini, mashetani nk. Pia viumbe hivyo vimegewanyika katika makundi mawili kuna viumbe wema na wabaya kwahiyo imetokea umekumbana na kiumbe mbaya basi atakusumbua mpaka kufa kwako.. sasa mkasa huu wa kusisimua na kutisha unaelezea maisha ya viumbe hao na wanaadamu ambao wamejikuta wakiingia kwenye tabu kubwa sana ya kurumbana na viumbe hivyo....... Simulizi yetu inaanzia katika nyumba moja nzuri ya kifahari majira ya usiku nyumba ambayo tangu miaka 10 nyuma haikuwahi kukaliwa na mtu yeyote lakini nyumba hiyo licha ya kuto kukaliwa na mtu haikuchakaa wala kuchafuka muda wote ilionekana mpya machoni mwa watu.       Majira hayo kulionekana kuwa na vijana wanne waliokuwa wakikimbia huku mkononi wakiw...

USIKU WA KIFO (03)

Image
Jina.......Usiku Wa Kifo Mtunzi....Dully Official Tz WhatsApp....0752748344 Mkasa wa kutisha... Sehemu ya 03 ILIPOISHIA.. Mpenzi msomaji yaani asikwambie mtu usingizi wa hapo ulikuwa mtamu sana lakini nikiwa kwenye usingizi nilishtuka baada ya kuitwa kwa jina langu na nilipoamka sikuwaona wenzangu wote walikuwa wametoka nnje na vilio ndivyo vilikuwa vikisikika upande wa nnje....ENDELEA... Niliinuka haraka na kutoka nnje lakini sikuamini kuona damu zimetapakaa chini tena zilikuwa kwa mtindo wa kuburuzika kuashiria aliekufa alikuwa akiburuzwa kupelekwa sehemu nyingine. "Jamani kwani kuna nini na hizi damu ni zanani"      Niliuliza kwa hofu lakini sikujibiwa ila nilioneshwa ishara kwa kidole nitazame mbele na nilipotazama niliona nguo za dereva wetu zikiwa juu ya mti. "Mungu wangu ni nini tena hiki..!!?"        Hofu niliyokuwa nayo nilihisi kizungu zungu lakini tukiwa kwenye majonzi Tony alitushauri kitu. "Jamani mimi siamini kama kweli dereva wetu amekuf...

JERAHA LA MOYO (1)

Image
   Sehemu Ya 01 Mtunzi : Dully Tz WhatsApp :0752747344 Ilikuwa asubuhi na mapema siku ambayo Nelson alikuwa na furaha sana siku hiyo ilikuwa ni siku ambayo alikuwa akienda kuanza kidato cha kwanza baada ya kuhitimi elimu ya msingi na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya secomdary hivyo kwa siku hiyo alikuwa na furaha isiyo kifani. Aliamka majira ya saa kumi na moja subuhi na kujiandaa kisha alienda chumba cha mama yake na kusimama nnje ambapo alianza kubisha mrango. "Hodiii mama..!!?" Nelson aliita huku akiwa na shakuku kibao na kweli mama yake alifungua mrango na kumkuta tayari amejiandaa kama mwanafunzi. "Heeee jamani asubuhi yote hii hata shule wanafunzi hawajaanza kwenda wengine wanavuta mashuka wewe tayari umeshavaa na safari juu ya kutaka tuondoke" "Ndiyo mama sitaki kuchelewa mimi nikakosa dawati la kukalia" "Hahaha amna kwanza kule hakuna madawati kama shule ya msingi yaani kule unapewa kiti kila mmoja na chake' "Mh mama ila nataka kuwa...

USIKU WA KIFO (02)

Image
Jina......Usiku Wa Kifo Mtunzi....Dully Official Tz WhatsApp....0752748344 Mkasa wa kutisha... Sehemu ya 02 ILIPOISHIA.. Niliwaambia lakini wakina michael, Tony na Aron walianza kunibisha ila nilivyozidi kuwalazimisha ghafla tulisikia mrango wa kutokea ukifungwa taratibu na baada ya kufungwa tulisikia hatua za watu wakija kwenye chumba tulichokuwa sisi na hakuwa mtu mmoja maana hatua zilisikika nyingi sana kuashiria watu walikuwa zaidi ya mmoja....ITAENDELEA.. Hofu ilitutanda, kila mmoja alijificha nyuma ya mwenzake lakini muda huo huo tukiwa kwenye taharuki ghafla zile hatua za viatu zilitulia na mrango tulisikia ukifunguliwa. "Jamani inabidi tutoke humu tena kwa tahadhari la sivyo tutajikuta tunaishia humu humu haya mnifuate"         Tony ambae ndiye kiongozi wa safari aliwasha tochi yake na kutangulia kutoka huku wengine tukifuata nyuma lakini mimi ndiye nilikuwa wa mwisho kabisa nilimkamata shati kwa nguvu Sara ambae nae pia alionekana kuwa muonga kama mimi. "Rai...