USIKU WA KIFO (02)


Jina......Usiku Wa Kifo

Mtunzi....Dully Official Tz

WhatsApp....0752748344

Mkasa wa kutisha...


Sehemu ya 02


ILIPOISHIA..


Niliwaambia lakini wakina michael, Tony na Aron walianza kunibisha ila nilivyozidi kuwalazimisha ghafla tulisikia mrango wa kutokea ukifungwa taratibu na baada ya kufungwa tulisikia hatua za watu wakija kwenye chumba tulichokuwa sisi na hakuwa mtu mmoja maana hatua zilisikika nyingi sana kuashiria watu walikuwa zaidi ya mmoja....ITAENDELEA..



Hofu ilitutanda, kila mmoja alijificha nyuma ya mwenzake lakini muda huo huo tukiwa kwenye taharuki ghafla zile hatua za viatu zilitulia na mrango tulisikia ukifunguliwa.


"Jamani inabidi tutoke humu tena kwa tahadhari la sivyo tutajikuta tunaishia humu humu haya mnifuate"

        Tony ambae ndiye kiongozi wa safari aliwasha tochi yake na kutangulia kutoka huku wengine tukifuata nyuma lakini mimi ndiye nilikuwa wa mwisho kabisa nilimkamata shati kwa nguvu Sara ambae nae pia alionekana kuwa muonga kama mimi.


"Raiyan hebu niachie huko utaniangusha jamani uwoga gani huo tunakamatana kama wafungwa.!"

     Sara aliongea kwa gadhabu huku akiitoa mikono yangu iliyoshika vyema shati lake.


"Shiiiii..!!! hebu nyamazeni jamani hamuoni kama tupo hatarini je kama kuna watu wabaya si mnawashtua na kujikuta tukifia humu humu"

       Aron aliongea kwa sauti ya chini huku nae akiwa makini kutazama mbele kiufupi wote hakuna ambae mwenye nafuu kila mmoja alijawa na woga moyoni mwake.


Tulifanikiwa kutoka kwenye jengo hilo la kanisa na baada ya kutoka nnje hakuna aliesuburi Tony atangulie tena kila mmoja alikimbia kuwahi lilipo gari lakini tulipolifikia tulibaki midomo wazi baada ya kuto mkuta dereva.


"Jamani huyu dereva ameenda wapi mbona anataka tuanze kulia"

       Betina alianza kulengwa na machozi huku akiangaza macho yake pande zote na muda huo wote tulikuwa tayari tumeingia kwenye gari na kufunga mrango.


"Jamani nipo nipo msiwe na wasi nilienda kuchimba dawa kidogo maana nilibanwa na haja lakini nipo msijali"

      Wote tulishusha pumzi baada ya kusikia sauti ya dereva na kweli tulipochungulia nnje tulimuona akirudi kutokea porini huku akifunga zipu yake ya suruali.


"Jamani mbona umetutia presha dereva ujue bado kidogo nikalie usukani niendeshe"

     Salome aliongea kwa utani huku akifungua begi lake na kutoa makeup ili kijiremba vizuri.


"Haya sasa mama kujiremba sijui usiku huu anajiremba amvutie nani au unataka uwavutie mashetani waliokuwa huku"

      Michael alimtania Salome na muda huo gari tayari ilikuwa imeng'oa nanga kutokomea mbele zaidi.


Safari ilizidi kwenda mbele ulipofika muda wa kula tulipaki gari pembeni na dereva alikuja upande wa nyuma ili kujumuika nasi kupata chakula cha usiku muda huo saa zilisoma saa 4: kamili usiku.


"Hivi dereva nataka kukuuliza kitu kama hutajali lakini samahani pia kwa kuuliza swali huku ukiwa unakula"

     Nilivunja ukimya na watu wote walibaki kunisikiliza mimi nilitaka kumuuliza nini dereva kwa muda huo.


"Usijali Raiyan wewe uliza kuwa huru"

       Dereva baada ya kunipa ruhusa alikaa makini kusikiliza swali langu.


"Hivi nataka kuuliza wakati sisi tumeenda kwenye lile kanisa na kuingia ndani hukuona kitu chochote cha tofauti kinaendelea?"

     Swali langu lilimfanya dereva agune kidogo kisha alinijibu.


"Hapana sijaona kitu maana nyie mlipoingia kwenye lile kanisa nilifunga mirango, nilitegesha alarm ya dakika tano na kulala zangu kwani kuna nini mimetokea"


"Ok basi usijali nilifikiri umeona kitu chochote lakini kama hujaona kitu vizuri ila muda mwingine usifunge mirango maana tunaweza kukuta vitu vya tofauti kwenye uchunguzi wetu tukakimbilia gari kumbe mwenzetu umefunga mirango mwisho ikawa balaa"


"Ok sawa nimewalewa"


Baada ya kuzungumza machache na dereva tulimalizia kula na safari ilianza kuelekea mbele zaidi ili kujifunza mengi na kuweka kumbukumbu maishani mwetu.


                              *********


Kila sehemu iliyokuwa na jengo kubwa lililoandikwa kwenye kitabu basi tulishuka na kwenda kujifunza yaliyomo humo kisha kurudi na kuendelea safari yetu lakini kwenye safari yetu tulifika sehemu hatukuona muelekeo wa barabara zaidi ya sauti za maji tu yakitiririka ilibidi tushuke na kuangalia maji hayo yalikuwa yakitokea wapi na kuelekea wapi.


Wote tulishuka na kuwasha tochi zetu lakini tulipotazama kwa makini yale maji ulikuwa ni mto ila ulikuwa ukitiririsha maji yaliyokuwa na rangi ya kijani.


"Jamani mbona huu mto kama alitufundisha madam Zena unaitwa mto wa ahadi au sio huu"

      Niliongea na kufanya kila mmoja awashe tochi kumulika.


"Ni kweli Raiyan hata hujakosea ni mtu wa ahadi lakini madam Zena alisema maji hutokea mashariki kuelekea magharibi lakini mbona huu hutokea magharibi kwenda mashariki?"

      Michael alisogea yalipo yale maji na kuyachota kwa mkono lakini kitendo cha kuyachota yalibadilika na kuwa maji ya kawaida.


Kila mmoja alitoa simu yake na kurecodi tukio mwisho tulimaliza na kuvuka mto ule kwa miguu maana haukua na kina kirefu ambacho kingefanya tushindwe kuvuka.


Tulivuka na kusonga mbele huku kila mmoja akiwa na furaha lakini hatukuacha kubeba mabegi yetu ambayo yangeweza kutusaidia mbele ya safari.

     Wakati huu tuliongozana na dereva hatukutaka kumuacha pekeyake kwenye gari tuliongozana nae mwisho tulifika maeneo ya makaburi na kusimama.


"Jamani sasa tunatakiwa tuingie kwenye makaburi haya tukaangalie kaburi la Mr Clinton ambae ni muanzilishi wa mji huu na baada ya kutoka hapa tutaenda kwenye hospital aliyozaliwa Mr Clinton mwisho tutamalizia mwenye mapango ya kutisha"

       Tony alianza kuongoza kuingia kwenye makaburi hayo lakini wakati na mimi nataka kuingia nilimuona mtoto mdogo amesimama kwenye kaburi moja akinitazama.


Mtoto yule alikuwa mweusi na macho yake yalikuwa kama ya paka ila nilipofikicha macho na kutazama tena sikumuona, nilihisi huenda ni mawazo tu basi nilifuata na kuingia humo.


                            *********


Somo ketu la kujifunza kwenye makaburi hayo lilienda vizuri sana tulitafuta nyumba moja iliyokuwa tupu na kuingia.

     Nyumba hiyo ilitawala kiza kinene ilitupasa kuwasha moto na kukaa ili kujipumzisha na siku inayofuata tufanye somo letu kwa utulivu na kurudi chuo.


Story zilichukua muda mrefu mmoja baada ya mwingine alianza kupitiwa na usingizi lakini wakati na mimi naanza kupitiwa na usingizi nilimuona dereva wetu akiinuka na kutoka nnje.


Sikutaka kumuuliza wala kumsemesha nilimtazana mpaka alipoishia nilivuta shuka na kulala.

      Mpenzi msomaji yaani asikwambie mtu usingizi wa hapo ulikuwa mtamu sana lakini nikiwa kwenye usingizi nilishtuka baada ya kuitwa kwa jina langu na nilipoamka sikuwaona wenzangu wote walikuwa wametoka nnje na vilio ndivyo vilikuwa vikisikika upande wa nnje....ITAENDELEA...

      

Sasa unafikiri vilio hivyo vimetokana na nini au nini kimetoka hapo? basi tukutane sehemu ya 3 tujue nini kimetokea kwa vijana hao.


LIKE, SHARE KWA WINGI NILETE MUENDELEZO.... 



 

Comments

Popular posts from this blog

JERAHA LA MOYO (02)

JERAHA LA MOYO (1)

USIKU WA KIFO (03)