Jina....NYUMBA YA MAJINI
Mtunzi....Dully Official Tz
WhatsApp....0752747344

       Sehemu....01

        Katika maisha tunayoishi tunaishi na viumbe vingi sana ukiachana na viumbe vya kuonekana pia tunaishi na viumbe ambavyo havionekani kama majini, mashetani nk. Pia viumbe hivyo vimegewanyika katika makundi mawili kuna viumbe wema na wabaya kwahiyo imetokea umekumbana na kiumbe mbaya basi atakusumbua mpaka kufa kwako.. sasa mkasa huu wa kusisimua na kutisha unaelezea maisha ya viumbe hao na wanaadamu ambao wamejikuta wakiingia kwenye tabu kubwa sana ya kurumbana na viumbe hivyo.......

Simulizi yetu inaanzia katika nyumba moja nzuri ya kifahari majira ya usiku nyumba ambayo tangu miaka 10 nyuma haikuwahi kukaliwa na mtu yeyote lakini nyumba hiyo licha ya kuto kukaliwa na mtu haikuchakaa wala kuchafuka muda wote ilionekana mpya machoni mwa watu.
      Majira hayo kulionekana kuwa na vijana wanne waliokuwa wakikimbia huku mkononi wakiwa na begi dogo lakini vijana hao walipopita karibu na hiyo nyumba walisimama na kuanza kushauriana.

"Jamani kwani mnaonaje tukiingia humu kwenye hii nyumba tukagawana pesa zetu alafu kila mtu afuate mambo yake"
      Aliongea kijana mmoja mweupe na mrefu wa wastani aliefahamika kama Charles.

"Mh mimi siwashauri jamani kwani hamjawahi kusikia historia ya hii nyumba kuwa ina majini na watu waliowahi kuingia huku hawakutoka..!?"
    Kijana alieshika mkoba wa pesa alipinga wazo la Charles lakini wengine wawili waliobaki hawakutaka kumsikiliza walikubaliana na Charles na kuanza kuingia.

"Daniel acha nikwambie wewe kama hutaki tupe sisi huo mfuko wa pesa alafu kaa hapo nnje uone kama utaambulia kitu yaani ni muoga tu kama mwanamke hata mwanamke mwenyewe hawezi kuwa muoga kama wewe"
     Charles alimsogelea Danile na kuuchukua mfuko aliokuwa ameshika lakini Daniel baada ya kuona wenzake wanatokomea ndani hakutaka kukaa kizembea kukosa pesa aliwafuata na wote kwa ujumla waliingia humo.

Kitendo cha vijana hao kuingia kelele tu ndizo zilisikika na baada ya muda alionekana Danile akitoka kwa kujivuta maana mguu wake mmoja ulikuwa umekatwa na damu nyingi zilikuwa zikimtoka.

"Jamani msaadaaaa nakufaaaaa...!!?"

Danile alipaza sauti kuomba msaasa lakini hakupata msaada wowote ghafla walitoka wanawake wawili wenye uzuri sana na wanawake hao midomo yao ilionekana kutapakaa damu basi walimfuata Daniel kwa mwendo wa taratibu na baada ya kumfikia walimchukua na kurudi nae kwenye nyumba hiyo na ukimya ulitawala....

                             *******

Miaka 5 imepita tangu tukio la wale vijana kupotelea ndani ya ile nyumba basi jumaamosi moja tulivu mchana ndani ya fukwe za bahari kulikuwa na watu wengi sana na kwenye watu hao alionekana kijana mmoja smart akiwa ameketi mwenyewe huku akitazama mawimbi ya bahari yaliyokuwa yakitoka nchikavu na kurudi baharini.

Kijana yule kwa muonekano wa mkao wake alionekana kuwa mtu mwenye mawazo sana lakini akiwa kwenye dimbwi la mawazo alifika binti mmoja mrembo na kumshika bega.

"Samahani kakaangu naweza kupata kampani ya kukaa na wewe hapo?"
    Binti yule mrembo alimuongelesha kijana huyo lakini hakujibiwa yule kijana alionekana kuduwaa kumtazama na kumtafakari yule binti kwa uzuri wake.

Alikuwa ni binti fulani mweupe asiekuwa hata na doa usoni pia alikuwa na nywele ndefu zilizogusa mgungo wake na jinsi alivyoziachia zilifanya aonekane vizuri na kuwa kama binti wa kihindi.

"Samahani kakaangu naweza kuketi mbona unaonekana mwenye mawazo sana..!!?"

"ooh..!! samahani sana dah nilikuwa mbali kimawazo ila unaweza kuketi usiwe na wasi"

Binti yule baada ya kukubaliwa aliketi na kumtazama yule kijana kisha alimpa mkono na kujitambulisha kwa jina.

"Hellow mimi naitwa Rayna sijui nani mwenzangu?"
     Rayna baada ya kujitambulisha mkono wake ulipokelewa kwa heshima zote na hapo ikawa zamu ya yule kijana kujitambulisha.

"Aaa..aa naitwa Hamza yah ila nafurahi kukufahamu alafu una jina zuri sana yaani kulitamka uwe umekula na kushiba haswaa"

Hamza aliongea kwa utani na kunfanya Rayna atabasamu kitendo kilichonfanya aonekane mrambo zaidi lakini Hamza alipomtazama vizuri Rayna mdomoni aligundua jino lake moja lilikuwa refu sana ilibidi amuulize.

"Ah Hamza usijali kawaida ni jino la bandia tu nimeweka lakini kesho nitakwenda kulifanyia marekebisho likae vizuri usijali sawa"

"Ok sawa nipe atory maana naweza kusema wewe ndiye umekuja kunitoa mawazo niliyokuwa nayo"
      Hamza alikuwa muongeaji sana mpaka Rayna akivutiwa nae.

"Nilikuwa mbali nimekaa na dada yangu nimekuona upo na mawazo sana hivyo nikaona nije kukufariji kwahiyo usiwaze nipo kwaajili yako''

Hamza alijisikia furaha sana kusikia maneno hayo kutoka kwa binti mrembo kama Rayna na hapo hakutaka kulaza damu alitoa simu yake na kumuomba namba za simu.

"Mimi sina simu Hamza lakini nipe namba zako nikifika nitaazima simu ya dada nikupigie"

Hamza aliona hiyo fursa asiiache alimtajia namba Rayna japo hakuwa na simu lakini alizinakili na muda huo huo alifika mwanamke aliefanana sana Rayna lakini huyo alikuwa na kidoti cheusi puani.

"Hamza huyu ni dada yangu anaitwa Raya na hapa nahisi amekuja kunifuata tuondoke lakini kama nilivyokuahidi nitakupigia"
     Rayna baada ya kumtambulisha dada yake kwa Hamza walisalimiana na kuagana kisha Raya na Rayna waliondoka zao lakini kitendo cha Hamza kugeuka pembeni na kuwatazama tena hakuwaona ila hakujali akichukulia kawaida.

Hamza alikaa sana kwenye fukwe hizo na ilipotimu majira ya saa 12 alifunga safari kurudi kwenye makazi yake ila mawazo yake yote siku hiyo yalihamia kwa Rayna.

                              *********

Siku zilizidi kukatika Hamza hakupokea simu yeyote kutoka kwa Rayna mpaka ikapelekea rafiki zake vijiweni waanze kumbeza kwa maneno ya kashfa.

"Hamza sasa mbona kimya tangu juzi umesema umepata mtoto mkali lakini hatuoni dalili zozote au umependa jini nini hahaha"
      Marafiki vijiweni hawakuacha kumcheka na kumsema Hamza lakini Hamza hakutaka kuwajibu ila mawazo yake yalikuwa kwa Rayna kwanini alimdanganya.

"Alafu sikia niwaambieni jamani kama nimependa jini au nimependa mzuka mniache kila mtu na maisha yake sikuwahi kumfuatilia mtu na mimi sitaki mnifuatilie kama hamniamini sawa"

Hamza alionga kwa hasira na jazba kubwa lakini wakati akiendelea kufoka alisikia sauti laini ya kike ikimwita kutoka upande wa pili ilibidi ageuka na hakumini kumuona Rayna maeneo yale.

"Raynaaa..!!?"

Hamza uvumilivu ulimshinda alimkimbilia Rayna na kumkumbatia hapo aliwaacha midogo wazi rafiki zake ambao walikuwa wakimbeza na kusema.

"Oya wanangu kumbe Hamza alikuwa akiongea kitu true dah! cheki mtoto yule sijui mwarabu au muhindi..!?"

"Yaani sijui kampata wapi ila tulikuwa tunambishia sana lakini kwa sasa katuziba midomo"

Rafiki wote wa Hamza hawakuwa na neno la kusema tena walibaki kumtazama Hamza ambae alikuwa akiishia na Rayna kuelekea walipopajua wao.

"Jamani Rayna mbona ulinidanganya kuwa utanitafuta lakini ukawa kimya mpaka rafiki walianza kunicheka"

"Samahani Hamza unajua ninapokaa ni nadra sana kutumia simu hua haturuhusiwi na wazazi wetu hata dada mwenyewe simu anatumia kwa mashaka sasa unafikiri ningekutafutaje..?"

"Basi sawa usijali rafiki yangu lakini nataka kupajua kwenu"
      Hamza kitendo cha kuongea maneno hayo Rayna alishtuka na kumgeuka huku sura yake ikionekana kufura kwa hasira.

"Rayna vipi..!! upo sawa kweli?"

"Ah amna usijali utapajua ila sio leo kesho maana leo itakuwa vibaya kwasababu wazazi wangu wapo lakini kesho nitakufuata"
      Rayna aliongea huku akijaribu kukontrol hasira zake na mpaka muda huo haikujulikana sababu maalum ya yeye kuchukia.

"Basi sawa kwa sasa unaelekea wapi..!!?"

"Hamza nilikua naelekea kwa shangazi sasa wakati napita nikakuona kwahiyo nikaona sio mbaya hata tukisalimiana".

"Basi vizuri nikutakie safari njema ila ukipata nafasi fanya juu chini tuongee"
     Hamza baada ya kuagana na Rayna alirudi walipo rafiki zake lakini muda huu hakuna alieongea wote wakikaa kimya kwa aibu.

                            *********

Rayna baada ya kumuaga Hamza alitoweka kama upepo na kutokea nnje ya nyumba kubwa ambayo nyumba hiyo ndiyo ilikuwa maarufu kwa kupotea watu na hata vijana waliopotea miaka 5 iliyopita walipotelea kwenye nyumba hiyo.

Nyumba ilitawala kiza tu na ndani ya nyumba hiyo kulisikika ngurumo za kutisha kuashiria viumbe vilivyokuwa vikikaa mule havikuwa viumbe vya kawaida.
    Lakini licha ya kutisha kwa nyumba hiyo Rayna aliingia bila wasi na kuelekea moja kwa moja alipo mwanaume mmoja ambae mwanaume huyo alikaa kwenye kiti kikubwa kilichopambwa kwa dhahabu na kupiga magoti.

"Baba kazi uliyonituma inakwenda kutimia lazima mtu unae muhitaji nitamleta tena nitamleta akiwa mzima"

"Ni vyema binti yangu sasa unaweza kwenda kuendelea na majukumu yako kama kawaida"
     Mzee huyo mwenye sura iliyojaa mikunjo na sauti ya kukwaruza alifurahi baada ya kupata taarifa hizo na kujikuta akisubiri kwa hamu sana kuona alichomuagiza binti take kikitimia.

Rayna alikuwa si binaadamu kama Hamza anavyofikiri ila alikuwa ni jini hatari ambae alifika kwenye maisha yake ili kumuangamiza na yote hayo anafanya kwaajili ya baba yake ambae ni mfalme wa majini wote.

Rayna baada ya kufikisha taarifa kwa baba yake aliongoza mpaka kwenye chumba kimoja ambacho alionekana mwanamke mmoja mzee amelala kitandani na kwa muonekano alionakana mgojwa wa muda mrefu.

"Mama unaendeleje?"
     Rayna alifika kwa yule mwanamke na swali lake la kwanza lilikuwa ni kumjulia hali.

"Naendelea vizuri tu binti yangu lakini kwa unachotaka kukifanya sikushauri kwanza fikiria binaadamu wamekukosea nini mpaka mmekuwa mkiwaangamiza kila siku alafu tambua ipo siku na nyie mtakufa sasa je mkifa mtakuwa kwenye hali gani hebu tafakari kwanza"

Rayna baada ya kuambia maneno hayo hakutaka kumjibu mama yake aliondoka na kuelekea chumbani kwake.

                               ********

Majira ya usiku yalipotimu Hamza alirudi kwenye chumba chake alichopanga na kupumzika lakini mawazo yake yalikuwa kwa Rayna.

"Hivi huyu Rayna mbona amekuwa mtu wa tofauti sana yaani nimemuuliza kuhusu kwenda kwao amekasirika au...."
      Hamza kabla hajamaliza alichokuwa akikiwaza ghafla alisikia sauti za kutisha dirishani kwake ilibidi ainuke haraka kwenda kuchungulia.

Alichungulia lakini hakuona mtu wala kitu chochote hii ilimpa mashaka sana ilibidi asogelee swith ya taa na kuwasha lakini kitendo cha kuwasha taa alihisi kushikwa mgongoni na papo hapo taa ilizima na ndani kukatawala kiza tupu....ITAENDELEA....

Unafikiri Hamza nini kimemkuta na ni mtu gani ambae anahitajika na mfalme wa majini (baba Rayna) na kwanini ila sina jibu kwa sasa tukutane sehemu ya 2


 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JERAHA LA MOYO (02)

JERAHA LA MOYO (1)

USIKU WA KIFO (03)